Sorry, you need to enable JavaScript to visit this website.
Skip to main content

Sanaa mbali ya ajira ni daraja la amani:UN

Kiswahili

Sanaa mbali ya ajira ni daraja la amani:UN

Na
2019-02-15
.

Picha: UN News Kiswahili/ Grece Kaneiya. Rose Luangisa mshiriki wa maonesho ya sanaa ya Umoja wa Mataifa yafahamikayo kama 'Sanaa kwa ajili ya amani' jijini New York Marekani.

Picha: UN News Kiswahili/ Grece Kaneiya. Rose Luangisa mshiriki wa maonesho ya sanaa ya Umoja wa Mataifa yafahamikayo kama 'Sanaa kwa ajili ya amani' jijini New York Marekani.
  1. Play Sanaa mbali ya ajira ni daraja la amani:UN

Pause

Mbali ya kuburudisha , kuelimisha na kuleta kipato kwa maelfu ya watu wanaoikumbatia, sanaa pia ni chachu ya kuchagiza amani kwakuwa inawaleta watu pamoja, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Sanaa ni moja ya mbinu zinazotumiwa na Umoja wa Mataifa kueneza amani na kuondoa migogoro kote duniani. Aidha Sanaa inatumika pia kama ajira. N amiongoni mwa wanaoitumia Sanaa kujipatia kipato ni Bi Rose Luangisa ambaye ni mtayarishaji wa maonesho ya vitu vya asili kutoka barani Afrika na mwaka huu wa 2019 ameshiriki katika maonesho ya Sanaa ya Umoja wa Mataifa yaliyopewa jina ‘Sanaa kwa ajili ya amani’ yakifanyika katika makao makuu ya umoja huo jijini New York Marekani. Baada ya maonesho hayo Bi Luangisa ameketi na UN News Kiswahili kuzungumzia suala hilo. Akizungumza nami ameanza kwa kuelezea watu wanavyofaidika na shughuli za Sanaa.

.