Sorry, you need to enable JavaScript to visit this website.
Skip to main content

Kuhusu sisi

Mti wa machweo nchini Kenya Safari, Afrika. Picha: Damian Patkowski
Mti wa machweo nchini Kenya Safari, Afrika. Picha: Damian Patkowski

Africa Renewal ni gazeti la kidijitali la Umoja wa Mataifa linaloangazia maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa ya Afrika. Tunaangazia changamoto zinazokabili bara hili na suluhisho za changamoto hizo zinazotolewa na Waafrika wenyewe, ikiwa ni pamoja na usaidizi wa Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa.

Kupitia gazeti la kidijitali la Africa Renewal na majukwaa ya mitandao ya kijamii, warsha za mtandaoni na vikundi vya vijana, uhusiano na vyombo vya habari, na juhudi zingine za ushirikiano na ushirika, tunawasilisha mtazamo mpya kuhusu Afrika unaoonesha vitendo chanya na matumaini, huku ukipinga maelezo hasi mara nyingi yenye mrengo hasi kuhusu Afrika.

Tunatangaza mafanikio ya Afrika katika kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu, makubaliano ya Paris kuhusu mabadiliko ya tabianchi na Ajenda ya Afrika ya mwaka 2063. Mada tunazoshughulikia zinajumuisha maendeleo endelevu, hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, kilimo, sauti za vijana, uwezeshaji wa wanawake, afya, Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA) na juhudi zingine za ushirikiano wa kikanda, teknolojia na uvumbuzi, amani na usalama, maendeleo ya kiuchumi na zaidi.

Tunatengeneza maudhui yetu wenyewe, tunatoa kazi kwa waandishi huru walioko katika nchi mbalimbali za Afrika, na kuchagua maudhui kutoka mfumo wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika, tukifanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Mshauri Maalum kuhusu Afrika (OSAA), Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Afrika (ECA), na Wakala wa Maendeleo wa Muungano wa Afrika (AUDA-NEPAD).

Vyombo vya habari vinakaribishwa kuzichapisha tena makala za Africa Renewal bila malipo, na kututambua kwa kutumia lugha ifuatayo: Taarifa hii ilichapishwa kwa mara ya kwanza na Africa Renewal.

Tufuate kwenye Facebook na Twitter @AfricaRenewal

Ili kupokea machapisho yetu moja kwa moja kwenye sanduku lako la barua pepe, jiandikishe kupokea jarida la kila mwezi la Africa Renewal kupitia kiungo hiki: https://bit.ly/AfricaNewsletter