Sorry, you need to enable JavaScript to visit this website.
Skip to main content

COVID-19 yaongeza chumvi katika kidonda cha LGBTI

Kiswahili

COVID-19 yaongeza chumvi katika kidonda cha LGBTI

Na
2020-05-18
.

Marafiki wawili wanaounga mkono haki za wapenzi wa jinsia moja wakiwa kwenye maandamano jijini New York, Marekani (2018)

UN News/Elizabeth Scaffidi
  1. Play COVID-19 yaongeza chumvi katika kidonda cha LGBTI

Pause

Hii leo dunia inaadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga chuki dhidi ya wapenzi wa jinsia moja, waliobadili jinsia na wale wenye wapenzi wa jinsia zote, IDAHOT, katika changamoto kubwa, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake wa siku hii ya leo 17 Mei.

Guterres amesema, “miongoni mwa athari kubwa za ugonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19, ni ongezeko la kuweko hatarini kwa watu wa kundi hilo au LGBTI. Tayari wakikabiliwa na ubaguzi, mashambulizi na kuuawa, kwa sababu tu ya wao ni nani na nani wameamua kumpenda, watu hao wanakabiliwa na unyanyapaa mkubwa kutokana na virusi vya Corona na pia kutokana na vikwazo wanavyopata wakati wakisaka huduma za afya.”

Katibu Mkuu amesema kuna ripoti ya kwamba maelekezo kuhusu COVID-19 yanatumiwa vibaya na polisi ili kulenga wapenzi wa jinsia moja au waliobadili jinsia na mashirika yao.

“Kadri janga hili linavyozidi kuibuka, Umoja wa Mataifa utaendelea kuangazia vitendo hivyo na vinginevyo pamoja na umuhimu wa kila mtu kulindwa na kujumuishwa katika hatua dhidi ya janga la Corona,”  amesema Katibu Mkuu.

Ametamatisha ujumbe wake akisema kuwa “kwa pamoja hebu na tuungane dhidi ya ubaguzi na kwa haki ya kila mtu kuishi huru na usawa katika utu na haki.”

.