Katika kuadhimisha siku ya kimatifa ya lugha ya mama, Umoja wa Mataifai unasema asilimia 43 ya lugha 6000 ambazo zinazungumzwa leo duniani ziko hatarini kutoweka. Na kwamba ni ni mamia kadhaa tu ya lugha ambazo zimepewa nafasi katika mifumo ya elimu na kutumika kwa umma na ni chini ya lugha 100 ambazo zinatumika katika mtandao wa kidijitali.
Licha ya hali hii lakini kuna baadhi ya jamii ambazo zinajivunia lugha ya mama na ni kawaida kusikia matangazo ya lugha za mama mbali mbali kupitia radio na hata televisheni, ni kwa mantiki hiyo nimezungumza na mmoja wa watangazaji wa lugha ya mama Gakenia Gakeni ambaye anatangaza kwenye moja ya radio nchini Kenya na amenielezea umuhimu wa siku ya leo
(SAUTI GAKENIA)
Na je vipi kuhusu dhana ya kwamba kutangaza na lugha za mama kunachangia katika kueneza ukabila
(SAUTI GAKENIA-2)
TAGS: Siku ya lugha ya mama, UN