Sorry, you need to enable JavaScript to visit this website.
Skip to main content

Chanjo ya kwanza na ya aina yake ya malaria inatoa matumaini katika kuukabili ugonjwa huu

Kiswahili

Chanjo ya kwanza na ya aina yake ya malaria inatoa matumaini katika kuukabili ugonjwa huu

Siku hii inayahusu Malaria Duniani– Aprili 25 – tunaangazia jinsi mpango wa jaribio la chanjo unavyoendelea Malawi

2021-04-26
Share

Seliya Lawrence na mwanawe was miezi kumi ambaye ashapokea chanjo ya tatu ya malaria...

WHO Malawi/ Hudson Kubwalo
  1. Play Chanjo ya kwanza na ya aina yake ya malaria inatoa matumaini katika kuukabili ugonjwa huu

Pause

Clara Magalasi, anayeishi katika kijiji mashambani karibu na Lilongwe, mji mkuu wa Malawi, aliamkia asubuhi mbaya ya mawingu meusi yaliyotishia mvua.

Kwake Bi. Magalasi, hali mbaya ya hewa haikumzuia kutembea kilomita 4 kuelekea Kituo cha Afya cha Chileka. Bintiye Grace Butawo, aliyetimu miezi 22, alikuwa anastahili kupata dozi yake ya mwisho ya chanjo ya malaria ya RTS,S. Anayafahamu vyema manufaa ya chanjo hiyo.

Ninafahamu kwamba mwanangu akipata dozi zote nne, chanjo hiyo itampa kinga zaidi dhidi ya malaria na malaria kali. Tangu Grace alipozaliwa hajawahi kuugua malaria, tofauti na wanangu waliougua malaria mara nyingi walipokuwa umri wake,” anasema Bi. Magalasi.

Ikiongezwa katika njia nyingine zilizopendekezwa kudhibiti malaria, chanjo ya RTS,S inaweza kupunguza maambukizi ya malaria miongoni mwa watoto kwa asilimia 40, na kupunguza malaria kali inayotishia maisha kwa asilimia 30.

Maendeleo ya chanjo ya majaribio: miaka miwili baadaye

Kwa sasa, Grace ni miongoni mwa takriban watoto 220,000 katika Malawi waliopata angalau dozi moja ya RTS,S ya chanjo ya malaria kupitia utaratibu wa kawaida wa kuchanja kama mojawapo ya mipango muhimu ya majaribio katika mataifa yaliyo kusini mwa Jangwa la Sahara unaoongozwa na Wizara za Afya za Malawi, Ghana, na Kenya, na kushirikishwa na Umoja wa Mataifa, kupitia Shirika la Afya Duniani (WHO), na kusaidiwa na washirika wa afya ndani ya mataifa, wa kikanda na wa kimataifa.

Nchini Malawi, malaria ni miongoni mwa maradhi hatari ya watoto wa chini ya miaka mitano, pamoja na kichomi na kuhara. Mashirika ya WHO na UNICEF yamekuwa yakishirikiana na mamlaka ya afya kukabili ugonjwa huu, kwa kuwa unaweza kukingwa na kutibiwa kwa urahisi ukigunduliwa mapema.

Na fursa ilipojitokeza miaka miwili iliyopita ya kuanzisha chanjo hiyo ya malaria katika mipango ya chanjo za watoto ulimwenguni, Malawi lilikuwa taifa la kwanza kushirikishwa, ikifuatiwa na Ghana kisha Kenya. Chanjo hiyo ilifanywa kwa awamu zilizolenga wilaya 11 nchini Malawi.

Kimataifa, zaidi ya nusu ya vifo vya watoto hutokea Afrika, na malaria ni chanzo kikuu cha vifo hivyo. Mwezi Januari 2016, WHO ilipendekeza utekelezwaji wa mpango wa majaribio wa chanjo ya malaria ya RTS,S kwa watoto pamoja na mipango mingine ya kudhibiti malaria katika maeneo ya maambukizi wastani-hadi-ya juu ya virusi hivi. Chanjo hii ya malaria ndiyo ya kwanza, na hadi sasa, ya pekee inayoweza kupunguza malaria miongoni mwa watoto kwa kiasi kikubwa.

Uwezo wa chanjo kuimarisha usawa wa afya

Ili kupunguza vifo vya watoto, tunaweza kurejelea uwezo wa hatua kama chanjo ya malaria kutoa kinga zaidi katika chanjo fanifu ya watoto au jukwaa la EPI linalofikia takriban asilimia 80 ya watoto nchini. Chanjo hii inatoa kinga zaidi kwa watoto dhidi ya malaria.

Clara Magalasi na mwanawe Grace Butawo nyumbani kwake Lilongwe. Mtoto wake amepokea chanjo cha malaria na sasa ana uwezo zaidi wa kujikinga na ugonjwa© Photo: WHO Malawi/ Hudson Kubwalo.

Ni njia ya ziada kwa pamoja na neti zilizotibiwa (au neti za vitanda) na pia ni fursa ya kuwafikia watoto ambao hawajaanza kutumia neti za vitanda au njia nyinginezo za kuzuia malaria kinga ya malaria yaweza kuimarisha usawa katika kupata hatua muhimuza kuokoa maisha kutokana na malaria,” anasema Dkt. Nonhlanhla Dlamini mwakilishi wa WHO nchini Malawi.

Wizara ya Afya ya Malawi ikisaidiwa na mashirika ya UNICEF pamoja na WHO imeweka hatua za kudhibiti malaria kama vile neti zilizotibiwa (ITNs) pamoja na kunyunyizia kuta za nyumba viua wadudu (IRS). Hata hivyo, bado kuna kaya zilizo maeneo magumu kufikia ambazo hazijanufaika na hatua kama hizi.

Kama Seliya Lawrence, ambaye pia anatokea eneo la mashambani la Lilongwe, asemavyo, kaya yake haikupata viua wadudu ila mwanawe wa miezi 10 amepata dozi 3 za chanjo ya malaria kufika sasa.

Ninafahamu IRS ila mpango huo haukufika katika eneo letu. Ninashukuru kwamba mwanangu anapokea chanjo ya malaria inayoweza kumlinda kutokana na aina mbalimbali za malaria,” anasema Bi. Lawrence.

Uwezekano wa manufaa mengine: upungufu wa wanaolazwa hospitalini, ziara zaidi za ulinzi hospitalini

Ziara za hospitalini pamoja na kulazwa kwa sababu ya malaria zilikuwa zimewatwiga mzigo wa kifedha walio hatarini. Katika nchi ya Malawi, karibu asilimia 60 ya watoto wagonjwa wanaozuru vituo vyaa afya ni kwa sababu ya malaria. Data kutoka Kituo cha Afya cha Chileka katika Lilongwe zinaonyesha punguo la wagonjwa wa kulazwa kutokana na malaria miongoni mwa watoto chini ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwa chanjo hiyo. Wahudumu wa afya wanasema kwamba labda punguo hilo latokana na chanjo ya malaria.

Tangu kuanzishwa kwa chanjo ya malaria, yamkini imeweza kufaulu kuwaweka watoto wengi nje ya hospitali,” anasema Madalitso Chadewa, Msaidizi Mchunguzi Mkuu wa matibabu Kituo cha Afya cha Chileka.

Bi. Chadewa anasema kwamba jaribio hilo pia limeimarisha wanoaenda kwa chanjo za kawaida. Kabla ya jaribio hilo, kina mama wengi wangeziwacha ziara za watoto chini ya miaka mitano katika zahanati pindi watoto wao walipopata chanjo ya mwisho ya ukambi wakiwa na miezi 15. Lakini chanjo ya malaria imeongeza kipindi cha chanjo hadi umri wa miezi 22.

Watoto wanapokuja wakiwa na umri wa miezi 22, mbali na kuwapa dozi ya nne ya RTS,S, pia tunakagua ukuaji na uchunguzi mwingine wa jumla wa afya. Ukaguzi huu ni muhimu kwa kuwa unasaidia kugundua hatari za kiafya zinazoweza kuzuiwa miongoni mwa watoto wa chini ya miaka mitano,” aliongeza.

Jaribio la chanjo ya malaria katika muktadha wa COVID-19

Umoja wa Mataifa umekuwa ukiisaidia Wizara ya Afya ya Malawi kuhakikisha mwendelezo wa chanjo muhimu pamoja na huduma za malaria wakati wa janga la COVID-19, ikiwa ni pamoja na chanjo za malaria katika wilaya ambamo majaribio yanafanywa. Jaribio la chanjo ya malaria limeendelea bila kuchachawizwa kwingi.

Tunaelewa jinsi COVID-19 ilivyoweka shinikizo kwa mfumo wetu wa afya. Ni muhimu kwetu kuhakikisha kwamba huduma za chanjo za watoto, ikiwa ni pamoja na mpango wa chanjo ya malaria, zinaendelea wakati huu kwa sababu chanjo zinapunguza maradhi ya watoto, kuokoa maisha na kusaidia kuondoa shinikizo kwa mfumo wa afya,” asema Dkt. Randy Mungwira, afisa wa kiufundi wa WHO kuhusu mpango wa chanjo ya malaria nchini Malawi.

Hatua zifuatazo jaribio la chanjo ya malaria

Data na tajriba kutoka kwa chanjo ya malaria katika utekelezwaji wa jaribio itasaidia kuelewa njia bora za kuwafikia watoto na kanuni ya chanjo ya dozi nne, athari ya chanjo kwa malaria kali na kwa maisha yaliyookolewa, na usalama wa chanjo hiyo katika matumizi ya kawaida. Kwa sasa, data iliyopatikana kuhusu usalama inatoa hakikisho.

Jaribio linaendelea vyema, ukubalifu wa chanjo miongoni mwa wanajamii ni wa hali ya juu, na sasa mpango huo unaelekea katika udurusu wa data ya RTS,S uwezekano mkubwa wa WHO kupendekeza chanjo kwa matumizi mapana katika mataifa yaliyo kusini mwa Jangwa la Sahara mapema kama Oktoba 2021. Chanjo hiyo ikipendekezwa kwa matumizi mapana, inaweza kuwa nyongeza murua kwa mbinu zilizopendekezwa za kukabiliana na malaria, iliyopatikana kupitia jukwaa la chanjo ya watoto.

Mpango wa Utekelezaji Chanjo ya Malaria katika kanda ya Afrika unatokana na ushirikiano wa UN na Gavi, muungano wa Vaccine Alliance, Global Fund to Fight AIDS, Tuberculosis and Malaria, and Unitaid.

 

Kwa maelezo zaidi, tembelea malaria vaccine implementation programme website

 


Ms. Mukhuna works for WHO in Malawi

Share
.